Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

KUJIUNGA NA VYUO VYA TANZANIA BOFYA KATIKA PICHA

0 comments
KUJIUNGA NA VYUO VYA TANZANIA BOFYA KATIKA PICHA
Read More »

HOTUBU YA WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA YA KUAHIRISHA BUNGE

0 comments
PG4A9702
UTANGULIZI

a)    Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika,
1.    Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015.


2.    Napenda kutumia nafasi hii ya awali kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ya kutukuka ambayo wameifanya kwa nidhamu na ufanisi mkubwa, hususan wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Serikali na Mafungu ya Wizara za Kisekta. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi kwa kazi yao nzuri ya kuchambua Bajeti ya Serikali na Sheria zinazoambatana na masuala ya Bajeti. Changamoto zilikuwa nyingi,   lakini   kwa   pamoja   tumekubaliana   na   kuafikiana. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kwenda kushirikiana na Wananchi katika utekelezaji wa Bajeti hii ili kuwaletea maendeleo.

Mheshimiwa Spika,
3.    Katika kipindi hiki tukiwa hapa Bungeni, yapo matukio ya kusikitisha yaliyotokea ambapo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walipoteza Wapendwa wao. Aidha, yapo matukio ya Kitaifa yaliyosababisha kupoteza maisha ya Ndugu, Jamaa na Marafiki. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote waliofikwa na misiba na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wote waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki

Read More »

MAUAJI,,,Ni hatari chuo cha RUCO

0 comments
MAZISHI YA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA RUCO MWAKA WA NNE SHERIA ALIECHOMWA MOTO NA WANANCHI WAKIDHANIA YA KUWA NI JAMBAZI YANAFANYIKA LEO MOSHI ..INAUMA SANA KWA NDUGU JAMAA NA HATA WAZAZI AMBAO WALIKUWA WANAMTEGEMEA KWANI TAYARI ALIKUWA MWAKA WA MWISHO HIVYO MATUNDA YAKE YALIKUWA YANANGOJEWA LEO WANPOKEA MAITI YA MWANO TENAH AKIWA KACHOWA MOTO HAKUNA YEYOTE AMBAE HILI JAMBO HALIJAMGUSA ANDIKA NENO R.I.P KUMUOMBEA MAPUNZIKO MEMA KATIKA SAFARI HII YA MILELE YEYE AMETANGULIA SISI TUNAMFUATA HAKIKA INAUMA......tayari TIMU YA INFO IS HOT IMESHATEGA KAMERA ZAKE HUKO....

Read More »

BREAKING NEWS: AJALI MBAYA YATOKEA MAENEO YA MAKONGO NA KUSABABISHA VIFO

0 comments
http://theclicktz.com/


http://theclicktz.com/
Gari aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam imepata ajali mbaya leo mchana baada ya kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 18 katika eneo la Makongo Sekondari jijini Dar.
Inasikitisha Jamani ...RIP
By Pendo Lyimo

Read More »