VIONGOZ NDANI YA SABASABA...

Viongozi waipongeza kampuni ya TTCL Maonesho ya Sabasaba

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la TTCL katika maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Kibiashara katika viwanja vya Sabasaba. Mama Salma katika mazungumzo yake aliipongeza TTCL kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuleta maendeleo nchini.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la TTCL katika maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Kibiashara katika viwanja vya Sabasaba. Mama Salma katika mazungumzo yake aliipongeza TTCL kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuleta maendeleo nchini.
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Viongozi Waipongeza TTCL Maonesho ya Sabasaba
Viongozi Waipongeza TTCL Maonesho ya Sabasaba
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Baadhi ya wateja wa TTCL na wananchi wengine wakitembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la TTCL katika maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Kibiashara katika viwanja vya Sabasaba. Mama Salma katika mazungumzo yake aliipongeza TTCL kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuleta maendeleo nchini.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea Banda la TTCL katika maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Kibiashara katika viwanja vya Sabasaba. Mama Salma katika mazungumzo yake aliipongeza TTCL kwa kazi nzuri inayoifanya katika kuleta maendeleo nchini.
VIONGOZI mbalimbali wa Serikali waliotembelea Banda la Kampuni ya TTCL katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja wa Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba wameipongeza kampuni hiyo kwa utendaji kazi.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Mlengeya Kamani alimwaga pongezi hizo kwa TTCL alipotembelea banda hilo, ambapo aliipongeza Kampuni ya Simu TTCL kwa kazi nzuri ya kusimamia mawasiliano nchini. Kwa upande wake mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akitembelea banda la TTCL alipongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia sekta ya mawasiliano.
Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL ambayo pia katika maonesho hayo imefanikiwa kushinda tuzo katika kundi la kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, inashiriki katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Banda la TTCL limeendelea kuwa kivutio katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea ambapo wananchi wamekuwa wakifurika katika banda hilo kushuhudia bidhaa na huduma anuai zilizoletwa kwenye maonesho hayo.

 

KANISA LA TAG (TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD) LAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA 1300 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA

Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka vyandarua 1300 vya kukinga mbu waenezao Malaria kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tarehe 04/07/2014. Msaada huo ni sehemu ya vyandarua 8550 vitakavyotolea na Kanisa hilo kwa Mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa katika kuadhimisha  Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa hilo nchini. Pamoja na zoezi la ugawaji vyandarua hivyo maadhimisho hayo yataenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu na huduma mbalimbali za kiroho.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akizungumza katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ambapo amelishukuru kanisa hilo kwa mchango walioutoa wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya malaria. Ameziomba taasisi zingine binafsi kuiga mfano huo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini. Katika hatua nyingine amepiga marufuku matumizi mabaya ya vyandarua ikiwemo tabia ya kuzungushia kwenye bustani za mbogamboga ambapo amezitaka mamlaka husika kuwakamata watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua kali kutokomeza tabia hiyo.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano Ndugu Methew Sedoyyeka ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewataka viongozi wa Serikali na wananchi kuhamasishana kwenye shughuli za usafi na uhifadhi wa mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria na ugonjwa hatari wa Dengue. 
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya kukabidhi vyandarua 1300 kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa tarehe 04/07/2014. Alisema kuwa Kanisa la TAG lilizaliwa Igale Mkoani Mbeya mwaka 1939 na sasa  linaadhimisha Jubilee ya miaka 75 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Mungu anajali roho yako na mwili wako, jenga mahusiano nae”
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Mtika akifanya utambulisho wa wenyeji katika hafla hiyo.
Vyandarua 1300 vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa na Kanisa la TAG, vyandarua hivyo vitagawiwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizoainishwa Mkoani Rukwa. 
Picha ya pamoja.
- Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com

UZINDUZI WA MASHINE ZA ATM ZA SELCOM ZAFANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza kina mama waliotembelea kutoa pesa wakati wa uzinduzi wa mashine ya ATM ya kampuni hiyo ambazo zinatoa  pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu kama M-pesa,tigo pesa,Airtel Money, walipo tembelea katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere  kushoto ni Ester Kariwa na Joyce Mtema picha na mpiga picha wetu
Mmoja ya wateja waliotembelea banda la kampuni ya Selcom Wireless, Bi,Joriet Benjamin akichukuwa fedha zake katika ATM mashine mpya za kampuni hiyo wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere
Wafanyakazi wa Selcom kampuni ya Wireless, wakiwa katika banda lao wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere kutoka kushoto ni Juma Mgori Meneja ukuzaji biashara na masoko,Ofisa Mauzo Ally Mbaga na Meneja miradi wa kampuni hiyo Gallus Runyela

ATM mpya na za kisasa za selcom zawa kivutio kikubwa kwa kampuni ya selcom ambayo imekuwa ikijihusisha na utoaji wa malipo mbalimbali kama vile ving’amuzi na luku mwaka huu imezindua huduma yake mpya ya ATM ambazo zitakuwa zinatoa pesa kwa kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza Goerge Vupembe jinsi ya mashine zinavyofanya kazi
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Selcom Wireless  Ally Mbaga  kushoto akifurahia jambo na mteja, Bi, Rose Mombo aliyekuja kutoa pesa katika mashine ya ATM ya kampuni hiyo
Mtaalamu wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadhakitoa maherekezo ya jinsi ya kutumia mashine hizo
Meneja ukuzaji biashara na masoko kampuni ya Selcom Wireless Juma Mgori akionesha mashine hiyo

Mtaalamu wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadh akiwa katika moja ya mashine hizo zilizozinduliwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam
Meneja ukuzaji biashara na masoko
Juma Mgori akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashine za ATM za kampuni hiyo kwa ajili ya kutolea fedha
kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu mashine hizo za ATM
wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere

Rose Muhando kupeleka Pindo la Yesu Mwanza

images
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando anatarajia kutambulisha kwa mashabiki wake albamu ya Kamanda Pindo la Yesu Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.
Taarifa ya mwimbaji huyo kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa tayari mkoa wa Mwanza umekuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa Dar es Salaam.
“Nitazindua Diamond Jubilee Agosti 3, baada ya hapo nitaenda Mwanza Agosti 10 Uwanja wa CCM Kirumba, naomba mashabiki wangu wajiandae kupata vitu vizuri sana,
“Nimejipanga kuhakikisha nawapa burudani ya nguvu, najua nini wanakitaka, pia najua waimbaji gani wanawapenda, nipo katika utaratibu wa kuhakikisha wanafurahi,” alisema Muhando.
Kwa mujibu wa Muhando, nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.
Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAONYESHO YA TANTRADE LEO

1Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE yanayofanyika kila mwaka kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wakati alipotembelea na kukagua mabanda ya makampuni mbalimbali yanayoshiriki kwenye maonyesho hayo.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- DAR ES SALAAM 2Rais Jakaya Kikwete akielekea ofisini kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili  kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa TANTRADE leo, katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara na kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje TANTRADE  Bi. Anna Bulondo 5Rais Jakaya Kikwete akiangalia majiko ya mkaa katika moja ya mabanda ya Kenya 6Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Ofisa Mauzo Mwaandamizi wa kampuni ya Gold Finger Investiment Bi.Beatrice Kibanya wakati alipoteaembelea banda hilo. 8Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na baadhi ya vijana kwenye banda lao la Forever Living 10Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na baadhi ya vijana kwenye banda lao la Forever Living 1112Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw.Babar Hussain wa kampuni ya kuteneneza viatu ya Zubair Shoes. 13Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. Edwin Wekefield wa kampuni ya Mimic Craftis kutoka nchini Afrika kusini inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano. 14Mshauri Mwelekezi Kiwanda cha Helmet Jeshi la Magereza  Bw. Alferio Nchimbi akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu kofia bora za kujikinga waendesha pikipiki (Helmet)wakati alipotembelea katika banda la Mafereza  15Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje wakati alipotembelea katika banda hilo leo Mh. Rais Jakya Kikwete aliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa.  3Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa Mawasliano wa Umoja wa Mataifa (UN)wakati alipotembelea banda hilo leo na kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini. 4Rais Jakaya Kikwete akizungumza na vijana waliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa katika mafunzo ya ujasiriamali  wa tatu kutoka kulia nji Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa Mawasiliano wa umoja wa Mataifa (UN)
17 Rais Jakaya Kikwete akimsalimia  mtoto ambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati akitembelea katika mabanda mbalimbali kwenye viwanja vya Sabasaba leo.

RAIS KIKWETE ATAKA UBORA ZAIDI WA BIDHAA ZA TANZANIA

_MG_9420
Na  Magreth Kinabo – MAELEZO
Rais  Jakaya Kikwete  amewataka wafanyabiashara  nchini kuongeza juhudi za kuongeza ubora zaidi wa bidhaa zao ili ziweze kushindana na  zile za nje ya nchi.
Aidha Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya  Biashara ya Kimataifa  kwa kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na tofauti.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete  wakati  akitembelea leo  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“ Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo kwa ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu  mimi ni kuendelea kufanya ziwe vizuri zaidi,” alisema Rais Kikwete.
 Akitembelea banda la Jeshi la M,agereza, Rais Kikwete ambapo alijionea uzalishaji wa bidhaa za kilimo, alilitaka jeshil  hilo kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora cha kisasa.
 Katika ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania, Bidhaa za Tanzaniana mengineyo.

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA PSPF LEO

??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????Rais Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha wageni, huku akipatiwa maelezo na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonhyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam leo. ?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????Rais Jakaya Kikwete, akipokewa na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonhyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini. ?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????Rais Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonhyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam.

KONGAMANO LA TATHMINI YA MIAKA 13 YA UTEKELEZAJI WA SERA MPYA YA MAMBO YA NJE LAFANYIKA DAR ES SALAAM

Waziri wa Ardhi na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akitoa mchango wake katika Mada ya Ushirikiano wa Vijana katika vyama vya Siasa Kimataifa wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
Mwakilishi wa Mgeni Mualikwa Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Vijana waliohudhuria Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto,upande wake wa kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk.Telephory Kyaruzi,Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.(Balozi Joseph Sokoine alimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Bernard Membe ambaye alikuwa na hudhuru)
Wadau wakifuatilia kwa makini michango ya Mada zinazotolewa wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam akizungumzia suala la kukuza na kuendeleza Umoja wa Afrika na kukuza Umoja wa Kiuchumi ikiwa pamoja na kuunga mkono sera ya kutofungamana na upande wowote na kuwataka Vijana wasomi kusimamia na kuchangia maoni yao katika upatikanaji wa Itikadi ya nchi.

Mtumishi wa Mungu Askofu Isaya Joseph akifuatilia kwa makini Mada mbali mbali wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia waliohudhuria.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk Telephory Kyaruzi akiagana na Mwakilishi wa Mgeni mwalikwa Balozi Joseph Sokoine kwenye Viwanja vya Karimjee mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

1Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, leo Julai 5, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Mbogamboga aina ya Kabeji ilivyostaawi katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maelezo ya kitaalam toka kwa Mtaalam wa Bustani wa Jeshi la Magereza, Stafu Sajini, Nicolaus Sikazye(aliyeinama) alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza katika Bustani ya Magereza leo Julai 5, 2014 Jijini, Dar es Salaam.
4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maelezo  toka kwa Mtaalam wa Kilimo, Mrakibu wa Magereza, Uswege Mwakahesya(kushoto)  alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kiatu aina ya Buti ambacho kimetengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga Moshi, Kiwanda hicho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza. Rais Kikwete ametembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014  katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMADI ATEMBELEA WATOTO YATIMA

DSC_1185Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mwekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifa wakati alipokwenda kuwatembelea Watoto Mayatima wanaohudumiwa na Jumuiya hio Amani Mjini Zanizbar.Katikati ni Katibu Mkuu wa Jumuiya Farouk Hamad.
DSC_1200Watoto Mayatima wanaohudumiwa na Jumuiya ya MUZDALIFAT wakisoma kasda kumkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
DSC_1213Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea Zawadi ya Mas-haf kwa mtoto Khunayna Said kwa niaba ya Wototo wenziwe Mayatima wanao hudumiwa na Muzdalifat alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
DSC_1216Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi akipokea Zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya yaKiislam ya  Muzdalifat Farouk Hamadi alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
DSC_1217Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifa Abdalla Hadhar Bahasha yenye Sadaka kwa ajili ya Watoto yatima alipowatembelea watoto hao Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

WAJUMBE WA KAMATI YA MRADI WA UBORESHAJI WA KATA YA MAKONGO JUU WAKUTANA NA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI PROFESA ANNA TIBAIJUKA OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM

2Waziri Tibaijuka (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati ya wananchi ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa makazi Makongo Juu katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilimtembelea waziri huyo ofisini kwake kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya Kata ya Makongo.
4 Hapa Waziri Tibaijuka akiwaonesha wajumbe hao ramani ya Makazi ya Makongo Juu.
3Waziri Tibaijuka (Wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makongo Juu, Protas Tesha
5Waziri Tibaijuka akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe hao. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com)

WAKAZI MTO WA MBU NA WAFANYAKAZI WA HIFADHI YA ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA

DSC_0290Mahmoud Ahmad Arusha
Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani

WAKAZI HAO WA KATA YA MTO WA MBU waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko
DSC_0281Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbal;i wanaokuja kutembelea mbuga hizo
DSC_0285Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu

STARS YA MART NOOIJ YATUA NCHINI KUTOKEA GABORONE

1
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
 TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars  inatarajia kutua nchini kesho (julai 6) mwaka huu ikitokea nchini Botswana ili kuendelea na programu nyingine ya mazoezi.
 Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliweka kambi ya wiki mbili, mjini Gaborone kwa ajili ya kujiwinda na mechi dhidi ya Msumbaji  kuwania kupangwa hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
 Mechi hiyo muhimu kwa kocha wa Stars, Mholanzi, Mart Nooij itapigwa katika dimba la Taifa, julai 20 mwaka huu na wiki mbili baadaye mchezo wa marudiano utapigwa mjini Maputo nchini Msumbiji.
 Ikiwa ni sehemu ya kujipima ubavu, Stars ilicheza mechi ya kirafiki siku za karibuni na wenyeji wao Botswana na kuchapwa mabao 4-2.
 Mabao ya Taifa stars yalifungwa na Khamis Mcha `Vialli` na John Raphael Bocco `Adebayor`.
 Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

MBEYA CITY FC KUONESHANA KAZI NA `WAJELAJELA SOKOINE LEO, TIKETI ZA ELEKRONIKI KUTUMIKA

Mbeya-CityNa Baraka Mpenja, Dar es salaam
 BAADA ya mapumziko ya kutoona mechi za ligi kuu katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya, wapenzi wa soka leo hii watajikumbushia ladha ya soka kwa kuzishuhudia Mbeya City fc na Tanzania Prisons zikichuana vikali.
 Hii ni mechi maalum ya kajaribu mfumo wa tiketi za elekroniki katika dimba hilo na inatarajia kuanza majira ya saa 10 kamili jioni.
 Mbali na kuwa mechi ya kirafiki, pia itatoa fursa kwa wapenzi wa timu hizi kuona vikosi vyao wakati huu maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania bara yakiendelea kushika kasi.
 Kusoma bofya www.bkmtata.blogspot.com

UMONY APIGWA CHINI NA AZAM FC…LAKINI APATA CHAKE KAMA KAWA!

UmonyMshambuliaji Brain Umony (kushoto) ameachwa na Azam fc
Na Baraka Mpenja Dar es salaam
MABINGWA wa soka Tanzania bara, wana Lambalamba Azam fc wamevunja mkataba na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Brian Umony.
Umony hayupo kwenye mipango ya kocha mkuu wa klabu hiyo, Mcameroon, Joseph Marius Omog, hivyo uongozi umelazimika kuachana naye.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema Umony baada ya kuitumikia Azam kwa mwaka mmoja na nusu ama miwili, wameamua kuachana naye kwa amani na kumpati stahiki zake.
“Uongozi wa Azam umekaa na mchezaji huyo na kuvunja mkataba wake. Kwa maana hiyo amepata stahiki zake na amekwenda mbele katika maisha yake ya mpira”.  Alisema Jafar.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

GIGGS AWA DAKTARI WA SAYANSI…HESHIMA YAKO MKONGWE!

article-2681002-1F64070500000578-694_634x872Heshima: Gwiji wa Manchester United akipozi katika picha baada ya kupata digrii yake kwenye ukumbi wa  Victoria Hall mjini Bolton.
GWIJI wa Manchester United, amezawadia shahada ya heshima ya Udaktari na chuo kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake mkubwa aliotoa katika mchezo soka.
Giggs aliyestaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu uliopita amepokea udaktari wa sayansi kwa mchango wake mkubwa katika michezo kwenye mahafali ya chuo iliyofanyika ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton jana ijumaa mchana. 
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

NEYMAR KUIKOSOA UJERUMANI NUSU FAINALI, AKIMBIZWA HOSPITALI, SCOLARI ATHIBITISHA!

article-0-1F65C61600000578-538_634x274NYOTA wa Brazil, Neymar,  ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz Felipe Scolari.
Taifa mwenyeji limefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya mechi kumalizika kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar amekuwa akijikaza kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na majeruhi ya  goti, lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.
article-2681224-1F65C63700000578-205_634x417Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi ya mgongo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.  article-2681224-1F66B2F100000578-76_634x756Hapa machela: Neymar akitolewa nje ya uwanja kwa machela, huku akiwaacha mashabiki na taifa zima likiwa katika hofu kubwa.
Kusoma zaidi habari hii bofya www.bkmtata.blogspot.com

UNAYAKUMBUKA YA MARADONA NA GENTILE MWAKA 1982?, IKIWA IMEPITA MIAKA 32, FERNANDINHO VS RODRIGUEZ WAIRUDIA HISTORIA

article-0-1F65737800000578-529_638x361Mpira uko wapi? Fernandinho akimfanyia kitu mbaya  James Rodriguez kipindi cha kwanza katika mchezo wa leo mjini Fortaleza.
KATIKA fainali za mwaka 1982 njia pekee ya Italia kumzuia Diego Maradona ilikuwa ni kumpa jukumu maalum beki wa kati Claudio Gentile ili ale naye sahani moja mwanzo mwisho. 
Gentile alimfanyia faulo 23 Muargentina huyo namba 10 nchini Hispania na Italia walishinda mabao 2-1, huku wakiwaachia wapinzani wao kazi ya kuifunga Brazil katika mechi inayofuata ili wasonge mbele, kitu walichoshindwa kufanya.
Miaka 32 baadaye, kulikuwa na tukio kama hilo kwenye mechi ya Brazil dhidi ya  Colombia ambayo imepigwa usiku huu mjini Fortaleza na kushuhudia Fernandinho akipewa jukumu la kumbaka James Rodriguez kwa kila nafasi atakayocheza uwanjani.
article-0-1F6572B100000578-984_638x334Hali tete: Rodriguez akiugulia maumivu baada ya kufanyiwa faulo ya kwanza na  Fernandinho, mjini Fortaleza.
Katika dakika ya 14, kiungo huyo wa Manchester City alichuana vikali na Rodriguez katikati ya dimba akijaribu kumpokonya mpira na alimshika nyota huyo wa Monaco.
Kusoma zaidi tukio hili bofya www.bkmtata.blogspot.com

BRAZIL WAICHACHAFYA COLOMBIA 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI, LAKINI `MBUNGI` WALIYOPIGIWA NI HATARI!

article-2681056-1F65BFA200000578-434_634x422Beki wa Brazil,  David Luiz aliachia shuti kali la mpira wa adhabu na kufunga bao la pili na la ushindi.
ULIKUWA usiku mkubwa kwa Wabrazil wakishuhudia vijana wao wa Samba wakicheza mechi ngumu ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya timu ya Colombia.
Haikuwa rahisi kuwazuia Wabrazil waliokuwa na morali ya kushinda mechi ya leo na kuungana na Ujerumani iliyofuzu nusu fainali kwa kuifunga Ufaransa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.
Usiku huu kumekuwepo na maendeleo, shukurani kwa bao la mapema la Thiago Silva (dakika ya 7) lililowachanganya Colombia.
Ulikuwa mchezo mkali na wenye kasi kwa dakika zote 90, lakini bao la pili lililofungwa na David Luiz kwa shuti kali la mpira wa adhabu katika dakika ya 68 liliwaamusha Wabrazil kwa mara nyingine tena.
Alikuwa kijana mkali, James Rodriguez aliyeifungia Colombia bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 80, lakini yote kwa yote, Wacolombia ndio `bai bai` tena.
article-2681056-1F65B0BF00000578-404_634x428 Luiz akishangilia baada ya kufunga goli kwa shuti la mpira wa adhabu lililomuacha kipa wa Colombia, David Ospina akiambulia manyoya tu.
article-2681056-1F65B95E00000578-473_634x456David Luiz akimshukuru Mungu wake baada ya kufunga, huku Paulinho akimtazama kwa tabasamu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA LEO

1 (6)Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge)akitembelea leo maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
2 (5)Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge)akipata  maelezo leo   kuhusu bidhaa  mbalimbali  kutoka kwa Bi mkubwa  Juma kwenye banda la Zanzibar  katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kushoto  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
3 (4)Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge) akipokelewa  na Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa  wakati alipotembelea leo  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
5 (3)Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete  akiakiangalia aina za ungo   wakati alipotembelea leo  banda la  Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa  kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia  ni  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Sophia Mjema.
6 (1)Mke wa Rais Mama  Salma Kikwete  akipata maelezo kuhusu vitabu vya mchakato wa Rasimu ya  Katiba mpya  na vya sheria  kutoka kwa Theresia  Kinabo ,ambaye ni Afisa Tawala wa Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) (aliyenyoosha mkono)   na pembeni yake ni Benadeta Thomas  amabye ni Afisa  Sheria  wakati alipotembelea leo  banda la Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa  kwenye  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.
Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo.

UJERUMANI MWENDO MDUNDO, YAITANDIKA UFARANSA 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

article-2680846-1F64430B00000578-12_634x381UJERUMANI imekuwa nchi ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali katika fainali za mwaka 2014 mwaka huu nchini Brazil baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa.
Bao hilo pekee la ujerumani limefungwa na beki Mats Hummels. 
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

Anatafutwa na Ndugu zake

Jina: Dickson Samwel Mbiling’i
Umri miaka 27
Kabila: Mkinga
Dini: Mkristo
Maeneo anayopenda kutembelea:
Iringa, Mbeya, Dar es Salaam na Bagamoyo.
Mtajwa hapo juu anatafutwa na ndugu zake. Kwa mara ya mwisho alionekana nyumbani kwake Mwananyamala Mchangani jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ya  Julai 2, 2014.
Wajihi wake ni maji ya kunde mrefu kiasi mwembamba wa wastani. Msamaria mwema yeyote mwenye taarifa zake au atakayemuona popote anaombwa kuwasiliana na ndugu zake kwa namba:-
0754 477226-Moses Mbiling’i
0754 301095-Adrew Mwilingu
0757 000014-Bartholomew Mbiling’i
0784 890389-Ahadi Kakore.

Rais Kikwete akutana na Waziri wa Ulinzi wa China Jenerali Chang Wanquan Ikulu

D92A5139   
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea na kufanya mazunguzmo na Waziri wa Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan.Baadaye Jenerali huyo alimpa zawadi Rais Kikwete na wakapiga picha ya Pamoja(picha na Freddy Maro
D92A5180
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazunguzmo na Waziri wa Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan.
D92A5215
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan na viongozi wengine aliofiatana nao
D92A5146
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi wa China(picha na Freddy Maro
D92A5189
 Jenerali huyo akimpa zawadi Rais Jakaya Kikwete na kupiga  picha ya Pamoja(picha na Freddy Maro

Wanamichezo waliokuwa China kujiandaa na Mashindano ya Jumuiya ya Madola warejea nchini huku wakiwa na matumaini makubwa

MC1aBaadhi ya wanamichezo waliokuwa nchini China kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Jumuiya ya Madola wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam . MC1bMkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo akisukuma mzizigo ya baadhi ya makocha wa China waliombatana na Wanamichezo wa Tanzania waliokuwa China kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya Olympic yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu mjini Glasgow Scotland, Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda akimpokea mmoja wa wanamichezo hao mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. MC2aMkuu wa Msafara wa Makocha sita kutoka China Bw. Kangkai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Makocha hao wa kutoka China ndiyo ambao walikuwa wakiwafundisha wachezaji wa michezo ya Riadha, Ngumi na Mpira wa Mezani (Table Tennis) wanamichezo wa Tanzania waliokwemda nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Olympic mjini Glasgow Scotland. MC2bMkuu wa msafara wa wanamichezo kutoka Tanzania waliokuwa nchini China kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic Bw. Boniphace Kimisha akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. MC3 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo akizungumza na wanamichezo waliokuwa nchini china kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. MC4Pichani Makocha sita kutoka China waliombatana na timu ya wanamichezo wa Tanzania waliokuwa wameenda nchini China kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotaraji kuanza mapema mwishoni mwa mwezi huu mjini Glasgow Scotland.Makocha hao wanafundisha michezo ya Riadha, Ngumi na Table Tenisi. MC5aMkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo (wapili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na makocho kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam. MC5b Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bibi. Juliana Yasoda (mwenye gauni la kitenge) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na makocho kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalin – WHVUM

NAIBU WAZIRI PEREIRA SILIMA ATEMBELEA MAONYESHO SABASABA

PIX 1Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (wapili kushoto) akiingia katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano ya Serikali wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PIX 2Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kulia) akimsikiliza Ofisa wa Jeshi la Polisi Inspekta Rukia Kibwana wa Kitengo cha Maadili na Malalamiko Makao Makuu alipokuwa anatoa maelezo kuhusiana na kitengo hicho kinavyofanya kazi zake, wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  PIX 3aibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kushoto) akiisikiliza Bendi ya Jeshi la Polisi (Steel Band) wakati ilipokuwa inatoa burudani katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PIX 4Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Injinia Omary Bakari (kulia) akimfafanulia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima, jinsi SIDO inavyofanya kazi zake wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PIX 5aibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kulia) akimuuliza swali Ofisa wa Jeshi la Magereza kuhusiana na gharama na jinsi samani za ndani zilivyoweza kutengenezwa. Naibu Waziri Silima alitembelea Mabanda mbalimbali katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PIX 6Ofisa wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhani (kulia) akimpa maelezo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima jinsi idara hiyo inavyowahudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la idara hiyo katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. PIX 7Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (wapili kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara yake wanaohudumia wateja mbalimbali wanaotembelea Wizara hiyo na Taasisi zake katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

DHAMIRA YETU NI KUKIDHI MAHITAJI YA WATEJA YA KIBENKI NA YA KIFEDHA.

Pichani ni  Meneja wa Tawi lililopo ndani ya  maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar
,Bi. Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki hiyo.Bi.Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na huduma bora kabisa katika soko  kwa bei inayowezekana kulipa na viwango  vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa mwanahisa.
Amesma benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH,ambapo zaidi ya ATM 180 na mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa.
 Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bwa.Adalbert Alchard akizungumza
na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo
na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar.Pichani kushoto ni 
Afisa wa Benki hiyo,Bi Tuddy Lutengan.

WADAU WA ELIMU KUKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI CHANGAMOTO ZINAKABILI SEKTA HIYO.

f3ecShukuru-Kawambwa2
Na Immaculate Makilika- MAELEZO WADAU wa elimu nchini wanatarajiakuwa na kongamano ambalo litakuwa likijadili juu ya uboreshaji wa elimu nchini.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti  wa  Kamati ya Kongamano la Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Job Chaula amesema kuwa kongamano hilo litasaidia kutafuta mbinu kuhusu nini kifanyike kuboresha zaidi  elimu ya Tanzania.
Dkt. Chaula ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa kongamano kubwa linalotarajiwa kuleta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini.
Amesema kuwa sio wakati wa Watanzania kulalamikia  Serikali na badala yake wanapaswa wajitume ili kubadilisha hali iliyopo.
Dkt Chaula ameongeza kuwa elimu ya Tanzania  inakabiliwa na  changamoto nyingi, kama vile mtazamo wa hasi wa baadhi ya jamii wa kupenda kuwaoza mabinti wao wakiwa na umri mdogo na hivyo kuwanyima fursa ya elimu.
Naye Katibu wa Kamati ya Kongamano la Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Maulid Nkungu amesema kuwa  pamoja na changamoto hizo zinazoikabili Sekta ya elimu nchini,Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha elimu nchini.
Amesema kuwa ni wakati wa wadau kushirikiana na Serikali kuboresha elimu kwa kuweka nguvu za pamoja katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zitakabili elimu nchini.
Kongamano hilo litafanyika mkoa wa Dar es salaam litakalofanyika  tarehe 5/7/2014   Ubungo plaza .
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Elimu Tanzania,nini kifanyike”.

SHUKURANI KUTOKA FAMILIA YA Marehemu Lt. Col(Rtd)Maurice Noel Singano

 indexFamilia ya Bibi Mary Singano wa Sahare Tanga, inapenda kumshukuru Mungu kwa baraka na rehema zake katika kipindi cha msiba wa Marehemu Lt. Col(Rtd)Maurice Noel Singano kilichotokea tarehe 31/05/2014 Chennai, India .
Tunawashukuru Wizara ya Afya kwa msaada Wakati wa ugonjwa ,tunatoa shukrani  za kipekee kwa Mganga Mkuu wa Serikali Dr Donan Mmbando,Dr Goloka Muambata wa Tanzania nchini india na wote waliojitoa kuokoa maisha ya mpendwa wetu .
Tunamshukuru Dr. Jayashree ,Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Apollo Chennai kwa matibabu katika kipindi cha ugonjwa
Tunawashukuru father Maurusi, Jerome na father Francis  kwa huduma za kiroho, Watanzania waliokwepo Apollo katika kipindi Chote Cha  ugonjwa. Tunawashukuru Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Mathias Mlumba ,Jumuiya ya Mt Mathias Mtume wa Mikocheni DSM,Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Martha DSM na Mathias Mulumba Tanga. Baba Askofu jimbo la Tanga .Jumuiya ya Mt Yuda Thadei Sahare, Wawata na Walei Tanga.
Tunamshukuru Mkurugenzi wa St. Christina Bwana Gabriel Kessy, Mwenyekiti wa bodi ,Walimu,wafanyakazi na wanafunzi.Menejimenti na watumishi wa MSD,TFDA na Airtel kwa ushirikiano na kutufariji katika kipindi hiki kigumu. Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa huduma ya mazishi.
Tunawashukuru Ndugu jamaa,majirani na marafiki walioshirikiana nasi katika kipindi chote cha ugonjwa na msiba.Tumefarijika sana kwa upendo mlio tuonyesha na Mungu awabariki sana.
Kutakua na mkesha tarehe 25/07/2014 utakaohitimishwa na misa siku ya tarehe 26/07/2014 nyumbani kwa Bibi Mary Singano- Sahare Tanga. Wote mnakaribishwa
“Raha ya Milele umpee ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie,apumzike kwa AMANI”
“Nimepigana Vita vilivyo vizuri,nimeimaliza safari, imani nimeilinda” Timotheo 4:7

Waziri Nyalandu atembelea Idara ya Uwindaji wa Kitalii Arusha

4 Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa  Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini.
6Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akifurahia Keki iliyoandaliwa katika Chuo cha Taifa cha Utalii Arusha.
5Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu(wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa  Chuo cha Taifa cha Utalii kilichopo Sakina jijini Arusha na  Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini.

Rais Kikwete apokea hati za utambulisho ikulu kutoka kwa mabalozi wanne

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa.Mabalozi waliowasilisha hati zao leo ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Balozi Ismail Salem wa Malaysia,Balozi Georges Aboua wa Cote d’Ivore, Balozi Thony Fred Balza Arismendi wa Venezuela na Balozi Ahmat Awad Sakine wa Chad.Pchani mabalozi hao wakiwasilisha hati zao kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Huku Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma(Katikati) akishuhudia na kuongoza hafla hiyo.D92A4767Mhe.Ismail Salem Balozi wa Malaysia akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
D92A4863Mhe.Georges Aboua Balozi wa Cote d’Ivore akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
D92A4979Mhe.Thony Fred Balza Arismendi Balozi wa Venezuela akiwaasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
D92A5062Mhe Ahmat Awad Sakine Balozi wa Chad akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma(picha

0 comments: