Mwanamke uyu Arejesha shanga kanisani.... Jionee majabu hayaaa
Stori:MWANDISHI WETU, Arusha Katika
hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Asnath
Terevaeli hivi karibuni aliamua kukabidhi kanisani shanga za majini kwa
kile alichodai kuwa, zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.
Mwanamke
anayefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli akikabidhi shanga kwa
Mchungaji Kiongozi, (Frank Endrew) wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani
Arusha. Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kanisa la
Ufufuo na Uzima mkoani hapa baada ya moto wa Injili kuwashwa na
Mchungaji Kiongozi, Frank Endrew. Akizungumza
na Risasi Jumamosi, mmoja wa waumini wanaosali kanisani hapo
aliyejitambulisha kwa jina la Yusta John alisema, awali mwanamke huyo
alionekana mwenye jambo linalomtatiza na lilipotolewa tangazo la wenye
matatizo kupita mbele, Asnath alifanya hivyo huku akiwa ameshika shanga
mkononi. “Watu wengi walikuwa na shauku ya kujua lililomsibu mama huyo
lakini alipofika alimkabidhi mchungaji Frank shanga hizo
zilizotengenezwa kiasili zinazodaiwa ni za majini. “Mwenyewe alieleza
kuwa, alipewa kama zawadi na mwanaye lakini cha ajabu zimekuwa zikimtesa
na kumfanya akose amani.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
0 comments: