UTANGULIZI
a) Masuala ya Jumla
Mheshimiwa Spika,
1. Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015.
2. Napenda kutumia nafasi hii ya awali kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ya kutukuka ambayo wameifanya kwa nidhamu na ufanisi mkubwa, hususan wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Serikali na Mafungu ya Wizara za Kisekta. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi kwa kazi yao nzuri ya kuchambua Bajeti ya Serikali na Sheria zinazoambatana na masuala ya Bajeti. Changamoto zilikuwa nyingi, lakini kwa pamoja tumekubaliana na kuafikiana. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kwenda kushirikiana na Wananchi katika utekelezaji wa Bajeti hii ili kuwaletea maendeleo.
Mheshimiwa Spika,
3. Katika kipindi hiki tukiwa hapa Bungeni, yapo matukio ya kusikitisha yaliyotokea ambapo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walipoteza Wapendwa wao. Aidha, yapo matukio ya Kitaifa yaliyosababisha kupoteza maisha ya Ndugu, Jamaa na Marafiki. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote waliofikwa na misiba na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wote waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki
Read More »
Viongozi waipongeza kampuni ya TTCL Maonesho ya Sabasaba
by John Bukuku on July 6, 2014 in BIASHARA with No comments
VIONGOZI mbalimbali wa Serikali
waliotembelea Banda la Kampuni ya TTCL katika Maonesho ya 38 ya
Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja wa Mwalimu Julias
Nyerere, Sabasaba wameipongeza kampuni hiyo kwa utendaji kazi.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi, Dk. Titus Mlengeya Kamani alimwaga pongezi hizo kwa TTCL
alipotembelea banda hilo, ambapo aliipongeza Kampuni ya Simu TTCL kwa
kazi nzuri ya kusimamia mawasiliano nchini. Kwa upande wake mke wa Rais,
Mama Salma Kikwete akitembelea banda la TTCL alipongeza kwa kazi nzuri
wanayoifanya katika kuchangia maendeleo ya taifa kupitia sekta ya
mawasiliano.
Kampuni ya Simu Tanzania, TTCL
ambayo pia katika maonesho hayo imefanikiwa kushinda tuzo katika kundi
la kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, inashiriki katika Maonesho
ya 38 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba
jijini Dar es Salaam.
Banda la TTCL limeendelea kuwa
kivutio katika Maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea
ambapo wananchi wamekuwa wakifurika katika banda hilo kushuhudia bidhaa
na huduma anuai zilizoletwa kwenye maonesho hayo.
KANISA LA TAG (TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD) LAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA 1300 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA
by John Bukuku on July 6, 2014 in JAMII with No comments
Askofu
wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji
Nestory Watua akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew
Sedoyyeka vyandarua 1300 vya kukinga mbu waenezao Malaria kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tarehe 04/07/2014.
Msaada huo ni sehemu ya vyandarua 8550 vitakavyotolea na Kanisa hilo
kwa Mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa katika kuadhimisha Jubilee ya miaka
75 ya Kanisa hilo nchini. Pamoja na zoezi la ugawaji vyandarua hivyo
maadhimisho hayo yataenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu na huduma
mbalimbali za kiroho.
Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akizungumza katika hafla
hiyo fupi ya makabidhiano ambapo amelishukuru kanisa hilo kwa mchango
walioutoa wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya
malaria. Ameziomba taasisi zingine binafsi kuiga mfano huo kwa kuunga
mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini. Katika
hatua nyingine amepiga marufuku matumizi mabaya ya vyandarua ikiwemo
tabia ya kuzungushia kwenye bustani za mbogamboga ambapo amezitaka
mamlaka husika kuwakamata watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua kali
kutokomeza tabia hiyo.
Muwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika hafla hiyo fupi
ya makabidhiano Ndugu Methew Sedoyyeka ambae ni Mkuu wa Wilaya ya
Sumbawanga akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewataka viongozi wa
Serikali na wananchi kuhamasishana kwenye shughuli za usafi na uhifadhi
wa mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria na ugonjwa
hatari wa Dengue.
Askofu
wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji
Nestory Watua akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya
kukabidhi vyandarua 1300 kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa tarehe 04/07/2014.
Alisema kuwa Kanisa la TAG lilizaliwa Igale Mkoani Mbeya mwaka 1939 na
sasa linaadhimisha Jubilee ya miaka 75 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho
hayo ni “Mungu anajali roho yako na mwili wako, jenga mahusiano nae”
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Mtika akifanya utambulisho wa wenyeji katika hafla hiyo.
Vyandarua
1300 vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa na Kanisa la TAG,
vyandarua hivyo vitagawiwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati
zilizoainishwa Mkoani Rukwa.
Picha ya pamoja.
- Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com
UZINDUZI WA MASHINE ZA ATM ZA SELCOM ZAFANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA
by John Bukuku on July 6, 2014 in BIASHARA with No comments
Wafanyakazi wa Selcom kampuni ya Wireless, wakiwa katika banda lao wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere
kutoka kushoto ni Juma Mgori Meneja ukuzaji biashara na masoko,Ofisa
Mauzo Ally Mbaga na Meneja miradi wa kampuni hiyo Gallus Runyela
ATM
mpya na za kisasa za selcom zawa kivutio kikubwa kwa kampuni ya selcom
ambayo imekuwa ikijihusisha na utoaji wa malipo mbalimbali kama vile
ving’amuzi na luku mwaka huu imezindua huduma yake mpya ya ATM ambazo
zitakuwa zinatoa pesa kwa kutumia mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel
Money, na Easy pesa ATM hizo zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada
ya kuziona kwa mara ya kwanza katika banda la Selcom na kushudia ATM
hizo mpya na za kwanza nchini kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za
mkononi
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza Goerge Vupembe jinsi ya mashine zinavyofanya kazi
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Selcom Wireless Ally Mbaga kushoto akifurahia jambo na mteja, Bi, Rose Mombo aliyekuja kutoa pesa katika mashine ya ATM ya kampuni hiyo
Mtaalamu wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadhakitoa maherekezo ya jinsi ya kutumia mashine hizo |
Meneja ukuzaji biashara na masoko kampuni ya Selcom Wireless Juma Mgori akionesha mashine hiyo
Mtaalamu
wa ufundi wa mashine za ATM za Selcom, Maful Awadh akiwa katika moja ya
mashine hizo zilizozinduliwa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es
salaam
Meneja ukuzaji biashara na masoko
Juma Mgori akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashine za ATM za kampuni hiyo kwa ajili ya kutolea fedha
kutumia
mitandao kama Mpesa,Tigo pesa,Airtel Money, na Easy pesa ATM hizo
zimevuta hisia nyingi kwa watanzania baada ya kuziona kwa mara ya kwanza
katika banda la Selcom na kushudia ATM hizo mpya na za kwanza nchini
kutumika kutoa pesa kwa njia ya simu za mkononi
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu mashine hizo za ATM
wakati wa
wakati wa
maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere
Rose Muhando kupeleka Pindo la Yesu Mwanza
by John Bukuku on July 6, 2014 in BURUDANI with No comments
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI mahiri nchini, Rose
Muhando anatarajia kutambulisha kwa mashabiki wake albamu ya Kamanda
Pindo la Yesu Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.
Taarifa ya mwimbaji huyo kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa tayari mkoa wa Mwanza umekuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa Dar es Salaam.
“Nitazindua Diamond Jubilee Agosti 3, baada ya hapo nitaenda Mwanza Agosti 10 Uwanja wa CCM Kirumba, naomba mashabiki wangu wajiandae kupata vitu vizuri sana,
“Nimejipanga kuhakikisha nawapa burudani ya nguvu, najua nini wanakitaka, pia najua waimbaji gani wanawapenda, nipo katika utaratibu wa kuhakikisha wanafurahi,” alisema Muhando.
Kwa mujibu wa Muhando, nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.
Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

RAIS JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAONYESHO YA TANTRADE LEO
by John Bukuku on July 5, 2014 in BIASHARA with No comments
Rais
Jakaya Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara
ya Kimataifa TANTRADE yanayofanyika kila mwaka kwenye viwanja vya
Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wakati
alipotembelea na kukagua mabanda ya makampuni mbalimbali yanayoshiriki
kwenye maonyesho hayo.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE- DAR ES SALAAM Rais
Jakaya Kikwete akielekea ofisini kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Maonyesho ya 38 ya Biashara
ya Kimataifa TANTRADE leo, katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa
Viwanda na Biashara na kulia ni Mkurugenzi wa Biashara ya Nje TANTRADE
Bi. Anna Bulondo Rais Jakaya Kikwete akiangalia majiko ya mkaa katika moja ya mabanda ya Kenya Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Ofisa Mauzo Mwaandamizi wa kampuni ya Gold Finger Investiment Bi.Beatrice Kibanya wakati alipoteaembelea banda hilo. Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na baadhi ya vijana kwenye banda lao la Forever Living Rais Jakaya Kikwete akipiga picha na baadhi ya vijana kwenye banda lao la Forever Living Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw.Babar Hussain wa kampuni ya kuteneneza viatu ya Zubair Shoes. Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. Edwin Wekefield wa kampuni ya Mimic Craftis kutoka nchini Afrika kusini inayojishughulisha na masuala ya mawasiliano. Mshauri
Mwelekezi Kiwanda cha Helmet Jeshi la Magereza Bw. Alferio Nchimbi
akitoa maelezo kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu kofia bora za kujikinga
waendesha pikipiki (Helmet)wakati alipotembelea katika banda la
Mafereza Rais
Jakaya Kikwete akipiga picha na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje
wakati alipotembelea katika banda hilo leo Mh. Rais Jakya Kikwete
aliwahi kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa
Kimataifa. Rais
Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Bi Hoyce Temu Mtaalamu wa
Mawasliano wa Umoja wa Mataifa (UN)wakati alipotembelea banda hilo leo
na kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo
hapa nchini. Rais
Jakaya Kikwete akizungumza na vijana waliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa
katika mafunzo ya ujasiriamali wa tatu kutoka kulia nji Bi Hoyce Temu
Mtaalamu wa Mawasiliano wa umoja wa Mataifa (UN)
RAIS KIKWETE ATAKA UBORA ZAIDI WA BIDHAA ZA TANZANIA
by John Bukuku on July 5, 2014 in BIASHARA with No comments
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Rais
Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara nchini kuongeza juhudi za
kuongeza ubora zaidi wa bidhaa zao ili ziweze kushindana na zile za nje
ya nchi.
Aidha Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kwa kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na tofauti.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete wakati akitembelea
leo maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye
viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“
Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo kwa
ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza
kushindana na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu mimi ni kuendelea
kufanya ziwe vizuri zaidi,” alisema Rais Kikwete.
Akitembelea
banda la Jeshi la M,agereza, Rais Kikwete ambapo alijionea uzalishaji
wa bidhaa za kilimo, alilitaka jeshil hilo kutoa elimu kwa wananchi juu
ya kilimo bora cha kisasa.
Katika
ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la
Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania, Bidhaa za
Tanzaniana mengineyo.
RAIS DR. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA PSPF LEO
by John Bukuku on July 5, 2014 in BIASHARA with No comments
Rais
Jakaya Kikwete, akisaini kitabu cha wageni, huku akipatiwa maelezo na
Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF,
Costantina Martin, alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonhyesho ya
38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya
Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam leo. Rais
Jakaya Kikwete, akipokewa na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na Masoko wa
Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea banda la
Mfuko huo kwenye maonhyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es
Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini. Rais
Jakaya Kikwete, akipatiwa maelezo na Meneja Mawasiliano, Uhusiano na
Masoko wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Costantina Martin, alipotembelea
banda la Mfuko huo kwenye maonhyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya
Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es
salaam.
KONGAMANO LA TATHMINI YA MIAKA 13 YA UTEKELEZAJI WA SERA MPYA YA MAMBO YA NJE LAFANYIKA DAR ES SALAAM
by John Bukuku on July 5, 2014 in SIASA with No comments
Waziri wa Ardhi na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akitoa mchango wake
katika Mada ya Ushirikiano wa Vijana katika vyama vya Siasa Kimataifa
wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya
ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto
lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai
5.2014.
Mwakilishi wa Mgeni Mualikwa Balozi Joseph Sokoine akizungumza na
Vijana waliohudhuria Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa
Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na
Changamoto,upande wake wa kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam Ndugu Ramadhani Madabida na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM
Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk.Telephory Kyaruzi,Kongamano hilo
lilifanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai
5.2014.(Balozi Joseph Sokoine alimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje
Mheshimiwa Bernard Membe ambaye alikuwa na hudhuru)
Wadau
wakifuatilia kwa makini michango ya Mada zinazotolewa wakati wa
Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo
ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika
kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam akizungumzia suala la kukuza na
kuendeleza Umoja wa Afrika na kukuza Umoja wa Kiuchumi ikiwa pamoja na
kuunga mkono sera ya kutofungamana na upande wowote na kuwataka Vijana
wasomi kusimamia na kuchangia maoni yao katika upatikanaji wa Itikadi ya
nchi.
Mtumishi wa Mungu Askofu Isaya Joseph akifuatilia kwa makini Mada mbali
mbali wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa
Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na
Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
salaam,Julai 5.2014.
Sehemu ya Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia waliohudhuria.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk Telephory Kyaruzi
akiagana na Mwakilishi wa Mgeni mwalikwa Balozi Joseph Sokoine kwenye
Viwanja vya Karimjee mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto.
RAIS KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
by John Bukuku on July 5, 2014 in BIASHARA with No comments
Kamishna
wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akimkaribisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Uwanja wa
Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, leo
Julai 5, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Mbogamboga aina ya Kabeji ilivyostaawi katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maelezo ya kitaalam toka kwa Mtaalam wa Bustani wa Jeshi la Magereza, Stafu Sajini, Nicolaus Sikazye(aliyeinama) alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza katika Bustani ya Magereza leo Julai 5, 2014 Jijini, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maelezo toka kwa Mtaalam wa Kilimo, Mrakibu wa Magereza, Uswege Mwakahesya(kushoto) alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kiatu aina ya Buti ambacho kimetengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga Moshi, Kiwanda hicho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza. Rais Kikwete ametembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMADI ATEMBELEA WATOTO YATIMA
by John Bukuku on July 5, 2014 in JAMII with No comments
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na
Mwekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifa wakati alipokwenda
kuwatembelea Watoto Mayatima wanaohudumiwa na Jumuiya hio Amani Mjini
Zanizbar.Katikati ni Katibu Mkuu wa Jumuiya Farouk Hamad.
Watoto Mayatima wanaohudumiwa na Jumuiya ya MUZDALIFAT wakisoma kasda kumkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipokea Zawadi ya Mas-haf kwa mtoto Khunayna Said kwa niaba ya Wototo wenziwe Mayatima wanao hudumiwa na Muzdalifat alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi akipokea Zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya yaKiislam ya Muzdalifat Farouk Hamadi alipowatembelea Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kulia akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifa Abdalla Hadhar Bahasha yenye Sadaka kwa ajili ya Watoto yatima alipowatembelea watoto hao Makao Makuu ya Jumuia Amani Mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
WAJUMBE WA KAMATI YA MRADI WA UBORESHAJI WA KATA YA MAKONGO JUU WAKUTANA NA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI PROFESA ANNA TIBAIJUKA OFISINI KWAKE DAR ES SALAAM
by John Bukuku on July 5, 2014 in JAMII with No comments
Waziri
Tibaijuka (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati ya wananchi ya
utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa makazi Makongo Juu katika Manispaa
ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ilimtembelea waziri huyo
ofisini kwake kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo ya
Kata ya Makongo.
Hapa Waziri Tibaijuka akiwaonesha wajumbe hao ramani ya Makazi ya Makongo Juu.
Waziri Tibaijuka (Wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo. Wa pili kushoto ni Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makongo Juu, Protas Tesha
Waziri Tibaijuka akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe hao. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com)

WAKAZI MTO WA MBU NA WAFANYAKAZI WA HIFADHI YA ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA
by John Bukuku on July 5, 2014 in JAMII with No comments
Mahmoud Ahmad Arusha
Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani
WAKAZI HAO WA KATA YA MTO WA MBU waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko
Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbal;i wanaokuja kutembelea mbuga hizo
Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu

STARS YA MART NOOIJ YATUA NCHINI KUTOKEA GABORONE
by John Bukuku on July 5, 2014 in MICHEZO with No comments
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Taifa ya
Tanzania, Taifa stars inatarajia kutua nchini kesho (julai 6) mwaka huu
ikitokea nchini Botswana ili kuendelea na programu nyingine ya mazoezi.
Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager iliweka kambi ya wiki mbili, mjini Gaborone
kwa ajili ya kujiwinda na mechi dhidi ya Msumbaji kuwania kupangwa
hatua ya makundi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya
Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo muhimu kwa kocha wa
Stars, Mholanzi, Mart Nooij itapigwa katika dimba la Taifa, julai 20
mwaka huu na wiki mbili baadaye mchezo wa marudiano utapigwa mjini
Maputo nchini Msumbiji.
Ikiwa ni sehemu ya kujipima
ubavu, Stars ilicheza mechi ya kirafiki siku za karibuni na wenyeji wao
Botswana na kuchapwa mabao 4-2.
Mabao ya Taifa stars yalifungwa na Khamis Mcha `Vialli` na John Raphael Bocco `Adebayor`.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
MBEYA CITY FC KUONESHANA KAZI NA `WAJELAJELA SOKOINE LEO, TIKETI ZA ELEKRONIKI KUTUMIKA
by John Bukuku on July 5, 2014 in MICHEZO with No comments
BAADA ya mapumziko ya kutoona
mechi za ligi kuu katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya,
wapenzi wa soka leo hii watajikumbushia ladha ya soka kwa kuzishuhudia
Mbeya City fc na Tanzania Prisons zikichuana vikali.
Hii ni mechi maalum ya kajaribu
mfumo wa tiketi za elekroniki katika dimba hilo na inatarajia kuanza
majira ya saa 10 kamili jioni.
Mbali na kuwa mechi ya kirafiki,
pia itatoa fursa kwa wapenzi wa timu hizi kuona vikosi vyao wakati huu
maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania bara yakiendelea kushika kasi.
Kusoma bofya www.bkmtata.blogspot.com
UMONY APIGWA CHINI NA AZAM FC…LAKINI APATA CHAKE KAMA KAWA!
by John Bukuku on July 5, 2014 in MICHEZO with No comments
Na Baraka Mpenja Dar es salaam
MABINGWA wa soka Tanzania bara, wana Lambalamba Azam fc wamevunja mkataba na mshambuliaji wao raia wa Uganda, Brian Umony.
Umony hayupo kwenye mipango ya kocha mkuu wa klabu hiyo, Mcameroon, Joseph Marius Omog, hivyo uongozi umelazimika kuachana naye.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar
Idd Maganga amesema Umony baada ya kuitumikia Azam kwa mwaka mmoja na
nusu ama miwili, wameamua kuachana naye kwa amani na kumpati stahiki
zake.
“Uongozi wa Azam umekaa na
mchezaji huyo na kuvunja mkataba wake. Kwa maana hiyo amepata stahiki
zake na amekwenda mbele katika maisha yake ya mpira”. Alisema Jafar.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
GIGGS AWA DAKTARI WA SAYANSI…HESHIMA YAKO MKONGWE!
by John Bukuku on July 5, 2014 in MICHEZO with No comments
Heshima:
Gwiji wa Manchester United akipozi katika picha baada ya kupata digrii
yake kwenye ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton.
GWIJI wa
Manchester United, amezawadia shahada ya heshima ya Udaktari na chuo
kikuu cha Bolton kutokana na mchango wake mkubwa aliotoa katika mchezo
soka.
Giggs aliyestaafu
kucheza soka mwishoni mwa msimu uliopita amepokea udaktari wa sayansi
kwa mchango wake mkubwa katika michezo kwenye mahafali ya chuo
iliyofanyika ukumbi wa Victoria Hall mjini Bolton jana ijumaa mchana.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
NEYMAR KUIKOSOA UJERUMANI NUSU FAINALI, AKIMBIZWA HOSPITALI, SCOLARI ATHIBITISHA!
by John Bukuku on July 5, 2014 in MICHEZO with No comments
NYOTA
wa Brazil, Neymar, ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji
dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz
Felipe Scolari.
Taifa mwenyeji limefanikiwa
kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini
Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela dakika tatu kabla
ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya mechi kumalizika
kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar amekuwa akijikaza
kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na majeruhi ya goti,
lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.
Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi ya mgongo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika. Hapa machela: Neymar akitolewa nje ya uwanja kwa machela, huku akiwaacha mashabiki na taifa zima likiwa katika hofu kubwa.
Kusoma zaidi habari hii bofya www.bkmtata.blogspot.com
UNAYAKUMBUKA YA MARADONA NA GENTILE MWAKA 1982?, IKIWA IMEPITA MIAKA 32, FERNANDINHO VS RODRIGUEZ WAIRUDIA HISTORIA
by John Bukuku on July 4, 2014 in MICHEZO with No comments
Mpira uko wapi? Fernandinho akimfanyia kitu mbaya James Rodriguez kipindi cha kwanza katika mchezo wa leo mjini Fortaleza.
KATIKA
fainali za mwaka 1982 njia pekee ya Italia kumzuia Diego Maradona
ilikuwa ni kumpa jukumu maalum beki wa kati Claudio Gentile ili ale naye
sahani moja mwanzo mwisho.
Gentile
alimfanyia faulo 23 Muargentina huyo namba 10 nchini Hispania na Italia
walishinda mabao 2-1, huku wakiwaachia wapinzani wao kazi ya kuifunga
Brazil katika mechi inayofuata ili wasonge mbele, kitu walichoshindwa
kufanya.
Miaka
32 baadaye, kulikuwa na tukio kama hilo kwenye mechi ya Brazil dhidi ya
Colombia ambayo imepigwa usiku huu mjini Fortaleza na
kushuhudia Fernandinho akipewa jukumu la kumbaka James Rodriguez kwa
kila nafasi atakayocheza uwanjani.
Hali tete: Rodriguez akiugulia maumivu baada ya kufanyiwa faulo ya kwanza na Fernandinho, mjini Fortaleza.
Katika
dakika ya 14, kiungo huyo wa Manchester City alichuana vikali na
Rodriguez katikati ya dimba akijaribu kumpokonya mpira na alimshika
nyota huyo wa Monaco.
Kusoma zaidi tukio hili bofya www.bkmtata.blogspot.com
BRAZIL WAICHACHAFYA COLOMBIA 2-1 NA KUTINGA ROBO FAINALI, LAKINI `MBUNGI` WALIYOPIGIWA NI HATARI!
by John Bukuku on July 4, 2014 in MICHEZO with No comments
Beki wa Brazil, David Luiz aliachia shuti kali la mpira wa adhabu na kufunga bao la pili na la ushindi.
ULIKUWA
usiku mkubwa kwa Wabrazil wakishuhudia vijana wao wa Samba wakicheza
mechi ngumu ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi ya timu ya Colombia.
Haikuwa
rahisi kuwazuia Wabrazil waliokuwa na morali ya kushinda mechi ya leo
na kuungana na Ujerumani iliyofuzu nusu fainali kwa kuifunga Ufaransa
bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.
Usiku huu kumekuwepo na maendeleo, shukurani kwa bao la mapema la Thiago Silva (dakika ya 7) lililowachanganya Colombia.
Ulikuwa
mchezo mkali na wenye kasi kwa dakika zote 90, lakini bao la pili
lililofungwa na David Luiz kwa shuti kali la mpira wa adhabu katika
dakika ya 68 liliwaamusha Wabrazil kwa mara nyingine tena.
Alikuwa
kijana mkali, James Rodriguez aliyeifungia Colombia bao la kufutia
machozi kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 80, lakini yote kwa yote,
Wacolombia ndio `bai bai` tena.
Luiz akishangilia baada ya kufunga goli kwa shuti la mpira wa adhabu lililomuacha kipa wa Colombia, David Ospina akiambulia manyoya tu.
David Luiz akimshukuru Mungu wake baada ya kufunga, huku Paulinho akimtazama kwa tabasamu.
David Luiz akimshukuru Mungu wake baada ya kufunga, huku Paulinho akimtazama kwa tabasamu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA LEO
by John Bukuku on July 4, 2014 in BIASHARA with No comments
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge)akitembelea leo maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge)akipata maelezo leo kuhusu bidhaa mbalimbali kutoka kwa Bi mkubwa Juma kwenye banda la Zanzibar katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati mwenye kitenge) akipokelewa na Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa wakati alipotembelea leo maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiakiangalia aina za ungo wakati alipotembelea leo banda la Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kuhusu vitabu vya mchakato wa Rasimu ya Katiba mpya na vya sheria kutoka kwa Theresia Kinabo ,ambaye ni Afisa Tawala wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) (aliyenyoosha mkono) na pembeni yake ni Benadeta Thomas amabye ni Afisa Sheria wakati alipotembelea leo banda la Mke wa Rais wa Awamu ya Tatu , Mama Anna Mkapa kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya sabasaba jijini Dares Salaam.

Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo.
UJERUMANI MWENDO MDUNDO, YAITANDIKA UFARANSA 1-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA
by John Bukuku on July 4, 2014 in MICHEZO with No comments
UJERUMANI
imekuwa nchi ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali katika fainali za
mwaka 2014 mwaka huu nchini Brazil baada ya kuibuka na ushindi wa bao
1-0 dhidi ya Ufaransa.
Bao hilo pekee la ujerumani limefungwa na beki Mats Hummels.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
Anatafutwa na Ndugu zake
by John Bukuku on July 4, 2014 in JAMII with No comments
Jina: Dickson Samwel Mbiling’i
Umri miaka 27
Kabila: Mkinga
Dini: Mkristo
Maeneo anayopenda kutembelea:
Iringa, Mbeya, Dar es Salaam na Bagamoyo.
Mtajwa hapo juu anatafutwa na
ndugu zake. Kwa mara ya mwisho alionekana nyumbani kwake Mwananyamala
Mchangani jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ya Julai 2, 2014.
Wajihi wake ni maji ya kunde mrefu
kiasi mwembamba wa wastani. Msamaria mwema yeyote mwenye taarifa zake
au atakayemuona popote anaombwa kuwasiliana na ndugu zake kwa namba:-
0754 477226-Moses Mbiling’i
0754 301095-Adrew Mwilingu
0757 000014-Bartholomew Mbiling’i
0784 890389-Ahadi Kakore.
Rais Kikwete akutana na Waziri wa Ulinzi wa China Jenerali Chang Wanquan Ikulu
by John Bukuku on July 4, 2014 in SIASA with No comments
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea na kufanya mazunguzmo na Waziri wa
Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan.Baadaye Jenerali
huyo alimpa zawadi Rais Kikwete na wakapiga picha ya Pamoja(picha na
Freddy Maro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazunguzmo na Waziri wa Ulinzi wa China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi wa
China na ujumbe wake Jenerali Chang Wanquan na viongozi wengine
aliofiatana nao
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi wa China(picha na Freddy Maro
Jenerali huyo akimpa zawadi Rais Jakaya Kikwete na kupiga picha ya Pamoja(picha na Freddy Maro
Wanamichezo waliokuwa China kujiandaa na Mashindano ya Jumuiya ya Madola warejea nchini huku wakiwa na matumaini makubwa
by John Bukuku on July 4, 2014 in MICHEZO with No comments
Baadhi
ya wanamichezo waliokuwa nchini China kwa ajili ya maandalizi ya
mashindano ya Jumuiya ya Madola wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam . Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo akisukuma mzizigo ya
baadhi ya makocha wa China waliombatana na Wanamichezo wa Tanzania
waliokuwa China kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na mashindano ya
Olympic yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu mjini Glasgow
Scotland, Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi.
Juliana Yassoda akimpokea mmoja wa wanamichezo hao mara baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam leo. Mkuu
wa Msafara wa Makocha sita kutoka China Bw. Kangkai akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Makocha hao wa kutoka
China ndiyo ambao walikuwa wakiwafundisha wachezaji wa michezo ya
Riadha, Ngumi na Mpira wa Mezani (Table Tennis) wanamichezo wa Tanzania
waliokwemda nchini humo kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Olympic
mjini Glasgow Scotland. Mkuu
wa msafara wa wanamichezo kutoka Tanzania waliokuwa nchini China kwa
ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic Bw. Boniphace Kimisha
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuwasili
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
leo. Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo akizungumza na wanamichezo
waliokuwa nchini china kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic,
mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Pichani
Makocha sita kutoka China waliombatana na timu ya wanamichezo wa
Tanzania waliokuwa wameenda nchini China kwa ajili ya maandalizi ya
mashindano ya Olympic yanayotaraji kuanza mapema mwishoni mwa mwezi huu
mjini Glasgow Scotland.Makocha hao wanafundisha michezo ya Riadha, Ngumi
na Table Tenisi. Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo (wapili kutoka
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji na makocho
kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bibi. Juliana Yasoda
(mwenye gauni la kitenge) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wachezaji na makocho kutoka china mara baada ya kuwasili katika Uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalin – WHVUM
Picha zote na Frank Shija,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalin – WHVUM
NAIBU WAZIRI PEREIRA SILIMA ATEMBELEA MAONYESHO SABASABA
by John Bukuku on July 4, 2014 in JAMII with No comments
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (wapili kushoto)
akiingia katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Mwasiliano ya Serikali wa Wizara hiyo, Isaac Nantanga.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kulia) akimsikiliza
Ofisa wa Jeshi la Polisi Inspekta Rukia Kibwana wa Kitengo cha Maadili
na Malalamiko Makao Makuu alipokuwa anatoa maelezo kuhusiana na kitengo
hicho kinavyofanya kazi zake, wakati wa Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya
Biashara ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. aibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kushoto) akiisikiliza
Bendi ya Jeshi la Polisi (Steel Band) wakati ilipokuwa inatoa burudani
katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Injinia
Omary Bakari (kulia) akimfafanulia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Pereira Silima, jinsi SIDO inavyofanya kazi zake wakati wa
Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea
Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi. aibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (kulia) akimuuliza
swali Ofisa wa Jeshi la Magereza kuhusiana na gharama na jinsi samani za
ndani zilivyoweza kutengenezwa. Naibu Waziri Silima alitembelea Mabanda
mbalimbali katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Ofisa
wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhani (kulia) akimpa maelezo Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima jinsi idara hiyo
inavyowahudumia wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la idara hiyo
katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima (wapili
kushoto-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara
yake wanaohudumia wateja mbalimbali wanaotembelea Wizara hiyo na Taasisi
zake katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba
yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
DHAMIRA YETU NI KUKIDHI MAHITAJI YA WATEJA YA KIBENKI NA YA KIFEDHA.
by John Bukuku on July 4, 2014 in BIASHARA with No comments
Pichani ni Meneja wa Tawi lililopo ndani ya maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar,Bi. Upendo Tendewa akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki hiyo.Bi.Upendo amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kukidhi mahitaji ya wateja ya kibenki na ya kifedha kwa kuhakikisha upatikanaji wa bidha na huduma bora kabisa katika soko kwa bei inayowezekana kulipa na viwango vyenye manufaa yanayolingana na gharama na faida ya kurudhisha kwa mwanahisa.

Amesma
benki hiyo inatumia kadi yako iitwayo Twiga ExpressCard ambayo mteja
anaweza kuitumia kupata huduma za kibenki katika ATM yoyote
iliyounganishwa na mtandano wa UMOJA SWITCH,ambapo zaidi ya ATM 180 na
mabenki ishirini nna nne nchini yameunganishwa.
Afisa Masoko wa Benki ya Twiga Bancorp Bwa.Adalbert Alchard akizungumza
na Wanahabari nje ya banda lao kuhusiana na huduma mbalimbali zitolewazo
na benki hiyo kwa wateja wao, kwenye maonyesho ya biashara ya Kimataifa
ya 38 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwal.Julius Nyerere jijini Dar.Pichani kushoto ni Afisa wa Benki hiyo,Bi Tuddy Lutengan.

WADAU WA ELIMU KUKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI CHANGAMOTO ZINAKABILI SEKTA HIYO.
by John Bukuku on July 4, 2014 in JAMII with No comments
Na Immaculate Makilika- MAELEZO
WADAU wa elimu nchini wanatarajiakuwa na kongamano ambalo litakuwa likijadili juu ya uboreshaji wa elimu nchini.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kongamano la Elimu Mkoa wa Dar es
Salaam, Dkt. Job Chaula amesema kuwa kongamano hilo litasaidia kutafuta
mbinu kuhusu nini kifanyike kuboresha zaidi elimu ya Tanzania.
Dkt.
Chaula ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na
waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa kongamano kubwa linalotarajiwa
kuleta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini.
Amesema kuwa sio wakati wa Watanzania kulalamikia Serikali na badala yake wanapaswa wajitume ili kubadilisha hali iliyopo.
Dkt
Chaula ameongeza kuwa elimu ya Tanzania inakabiliwa na changamoto
nyingi, kama vile mtazamo wa hasi wa baadhi ya jamii wa kupenda kuwaoza
mabinti wao wakiwa na umri mdogo na hivyo kuwanyima fursa ya elimu.
Naye
Katibu wa Kamati ya Kongamano la Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Maulid
Nkungu amesema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazoikabili Sekta ya
elimu nchini,Serikali imekuwa ikijitahidi kuboresha elimu nchini.
Amesema
kuwa ni wakati wa wadau kushirikiana na Serikali kuboresha elimu kwa
kuweka nguvu za pamoja katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zitakabili
elimu nchini.
Kongamano hilo litafanyika mkoa wa Dar es salaam litakalofanyika tarehe 5/7/2014 Ubungo plaza .
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni “Elimu Tanzania,nini kifanyike”.
SHUKURANI KUTOKA FAMILIA YA Marehemu Lt. Col(Rtd)Maurice Noel Singano
by John Bukuku on July 4, 2014 in JAMII with No comments
Familia
ya Bibi Mary Singano wa Sahare Tanga, inapenda kumshukuru Mungu kwa
baraka na rehema zake katika kipindi cha msiba wa Marehemu Lt. Col(Rtd)Maurice Noel Singano kilichotokea tarehe 31/05/2014 Chennai, India .
Tunawashukuru Wizara ya Afya kwa
msaada Wakati wa ugonjwa ,tunatoa shukrani za kipekee kwa Mganga Mkuu
wa Serikali Dr Donan Mmbando,Dr Goloka Muambata wa Tanzania nchini india
na wote waliojitoa kuokoa maisha ya mpendwa wetu .
Tunamshukuru Dr. Jayashree ,Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Apollo Chennai kwa matibabu katika kipindi cha ugonjwa
Tunawashukuru father Maurusi,
Jerome na father Francis kwa huduma za kiroho, Watanzania waliokwepo
Apollo katika kipindi Chote Cha ugonjwa. Tunawashukuru Paroko wa
Parokia ya Mtakatifu Mathias Mlumba ,Jumuiya ya Mt Mathias Mtume wa
Mikocheni DSM,Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Martha DSM na Mathias
Mulumba Tanga. Baba Askofu jimbo la Tanga .Jumuiya ya Mt Yuda Thadei
Sahare, Wawata na Walei Tanga.
Tunamshukuru Mkurugenzi wa St.
Christina Bwana Gabriel Kessy, Mwenyekiti wa bodi ,Walimu,wafanyakazi na
wanafunzi.Menejimenti na watumishi wa MSD,TFDA na Airtel kwa
ushirikiano na kutufariji katika kipindi hiki kigumu. Jeshi la wananchi
wa Tanzania kwa huduma ya mazishi.
Tunawashukuru Ndugu jamaa,majirani
na marafiki walioshirikiana nasi katika kipindi chote cha ugonjwa na
msiba.Tumefarijika sana kwa upendo mlio tuonyesha na Mungu awabariki
sana.
Kutakua na mkesha tarehe
25/07/2014 utakaohitimishwa na misa siku ya tarehe 26/07/2014 nyumbani
kwa Bibi Mary Singano- Sahare Tanga. Wote mnakaribishwa
“Raha ya Milele umpee ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie,apumzike kwa AMANI”
“Nimepigana Vita vilivyo vizuri,nimeimaliza safari, imani nimeilinda” Timotheo 4:7
Waziri Nyalandu atembelea Idara ya Uwindaji wa Kitalii Arusha
by John Bukuku on July 4, 2014 in BIASHARA with No comments
Watumishi
wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na
Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini ,wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo
,Lazaro Nyalandu leo kwenye ziara yake mkoani Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akisalimiana na Askari Wanyama Pori jijini Arusha leo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu(wa pili kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na
Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini.
Rais Kikwete apokea hati za utambulisho ikulu kutoka kwa mabalozi wanne
by John Bukuku on July 4, 2014 in SIASA with No comments
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa
mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa.Mabalozi waliowasilisha
hati zao leo ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Balozi Ismail Salem
wa Malaysia,Balozi Georges Aboua wa Cote d’Ivore, Balozi Thony Fred
Balza Arismendi wa Venezuela na Balozi Ahmat Awad Sakine wa Chad.Pchani
mabalozi hao wakiwasilisha hati zao kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
Huku Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma(Katikati) akishuhudia
na kuongoza hafla hiyo.Mhe.Ismail
Salem Balozi wa Malaysia akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu
wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.Mhe.Georges Aboua Balozi wa Cote d’Ivore akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Mhe.Thony Fred Balza Arismendi Balozi wa Venezuela akiwaasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma.
Mhe Ahmat Awad Sakine Balozi wa Chad akiwasilisha hati zake kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Katikati ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage Juma(picha
Read More »
Subscribe to:
Posts (Atom)